
Mkufunzi wa Arsenal amekubali kuondoka katika klabu hiyo mwisho wa msimu huu
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari Wenger amesema:
Baada ya kutafakari na kufanya mazungumzo na klabu , nahisi ndio wakati muafaka kujiuzulu mwisho wa msimu huu.
Nashukuru kwa kupata fursa ya kuihudumia klabu hii kwa miaka mingi.
Niliongoza klabu hii na moyo wangu wote pamoja na maadili.
Nataka kuishukuru wafanyikazi, wachezaji Mkurugenzi na mashabiki ambao wameifanya klabu hii kuwa maalum..
Nawaomba mashabiki wetu kuisaidia timu hii kumaliza msimu huu vizuri.
Kwa wapendwa wote wa Arsenal tunzeni maadili ya klabu hii.
'Naipenda na nitaishabikia maisha yangu yote'
Arsene Wenger
Post a Comment