Habari | Afya | Makala | Magazeti | Michezo | Burudani | Teknolojia | Mapenzi

Video Queen wa ngoma ‘Natamba’ Ya Aslay Akanusha Kutoka Nae Kimapenzi


Video Queen katika ngoma ya Aslay ‘Natamba’ amefunguka kuhusu taarifa za kutoka kimapenzi na muimbaji huyo.

Mrembo huyo ambaye pia aliwahi kutokea katika video ya Belle 9 na G Nako ‘Ma-Ole’ ameiambia The Base, ITV kuwa taarifa hizo hazina ukweli wowote kwani kwa sasa wao ni marafiki wa kawaida tu.

“Hapana, sijawahi kutoka na Aslay, wala hatujawahi kuwa na mahusiano ni rafiki yangu tu basi na tutaendelea kuwa marafiki wa karibu mengine no, sio marafiki wa karibu kiivyo,” amesema.

Natamba pengine ndio wimbo wa Aslay wenye mafanikio zaidi, wimbo hao hadi sasa katika mtandao wa Youtube una views zaidi ya Milioni 5 na hakuna wimbo wa Aslay uliofikisha idadi hiyo.
Labels:
Reactions:

Post a Comment

[facebook][blogger]

EYOPAH

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget