Habari | Afya | Makala | Magazeti | Michezo | Burudani | Teknolojia | Mapenzi

Tanzania itakuwa ya hovyo kuishi - Nape Nnauye


Mbunge wa jimbo la Mtama kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mh Nape Nnauye amefunguka na kusema kuwa kama nchi ya Tanzania viongozi wa kisiasa hawatajifunza kufanya siasa za kuvumiliana basi nchi itakuwa ya hovyo sana.
Nape Nnauye amesema hayo siku moja baada ya kuzikwa kwa mmoja wa Waasisi wa CHADEMA, Mzee Victor Kimesera na kusema kuwa kwake wanajifunza siasa za kuvumiliana 
"Pumzika Mzee Kimesera, kwako tunajifunza siasa za kuvumiliana! Viongozi wa kisiasa tusipojenga Utamaduni wa Kuvumiliana Tanzania itakuwa nchi ya hovyo kabisa kuishi" alisisitiza Nape Nnauye 
Mbali na hilo Nape Nnauye ametoa ujumbe wake wa Pasaka kwa wananchi wake wa Mtama na kuwataka kupendana na kushilikiana kwa ajili ya maendeleo ya jimbo lao la Mtama na kuhakikisha jimbo hilo linakuwa jimbo la mfano nchini. 
"Sikukuu hii ya Pasaka ikafufue ari ya kuendelea kupendana na kushirikiana katika kuhakikisha jimbo letu linakuwa la mfano nchini, kwa maendeleo , mafanikio , furaha na umoja bila kujali tofauti zetu mbalimbali. Nawatakia Pasaka njema" alisema Nape Nnauye 
Reactions:

Post a Comment

[facebook][blogger]

EYOPAH

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget