Habari | Afya | Makala | Magazeti | Michezo | Burudani | Teknolojia | Mapenzi

Rayvanny Afunguka Utendaji wa Kazi wa Daimond Ndani ya WCB


Msanii Rayvanny kutoka WCB amesema katika utendaji kazi wake na Diamond ndani ya label hiyo hawajawahi kufikia hatua ya kupishana kauli katika kazi.

Muimbaji huyo anayetamba na ngoma ‘Makulusa’ ameiambia Funiko Base ya Radio Five mara nyingi mambo yanayotokea ni ya kawaida ingawa kuna mengine huonyesha kutopendezwa nayo.

“Nikikosea lazima anikoromee lakini kunikoromea hajawahi kwa sababu yeye siyo mtu wa kufokafoka lakini kitu akikukataza unajua hiki kitu hajakipenda, kwa hiyo unajua wewe hapo inabidi ujiongeze,” amesema Rayvanny.

Soma Pia; Ujumbe wa Rayvanny kwa Diamond, ‘Hakuna anayefanikiwa akakosa maadui’

Rayvanny na Diamond wameshafanya ngoma pamoja inayokwenda kwa jina la Salome, pia wamekutana katika ngoma ‘Zilipendwa’ ambayo iliwakutanisha wasanii wote walio chini ya WCB. 
Labels:
Reactions:

Post a Comment

[facebook][blogger]

EYOPAH

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget