Habari | Afya | Makala | Magazeti | Michezo | Burudani | Teknolojia | Mapenzi

Mzee wa miaka 90 abaka watoto watano


Jeshi la polisi mkoani Shinyanga linamshikilia mzee Kachuka Malongo mwenye umri wa miaka 90, kwa tuhuma za kuwabaka wanafunzi watano wa shule ya msingi kwa nyakati tofauti tofauti.
Akizungumza na vyombo vya habari Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Simon Haule amesema kwamba wanafunzi hao ni wenye umri wa miaka minane hadi 12, na alikuwa akiwarubuni kwa kuwapa pipi na pesa, kutokana na uchu wa mapenzi aliokuwa nao.
“Tumebaini chanzo cha tukio hilo kuwa ni tamaa na uchu wa mapenzi, kwa hiyo tunamshikilia mtuhumiwa kwa mahojiano zaidi na uchunguzi ukikamilika tutampeleka mahakamani”, amesema Kamanda Haule.
Kamanda Haule aliendelea kwa kusema kwamba taarifa za watoto hao kufanyiwa vitendo hivyo vya ukatili walizipata kwa mkazi wa eneo hilo Amada Mganyizi, na ndipo walipoamua kuzifuatilia na kumkamata mtuhumiwa.
Pia Kamanda Haule amewataka wazai kuwa makini na karibu na watoto wao, ili kubaini matatizo yao au jambo lolote linapowatokea.
Reactions:

Post a Comment

[facebook][blogger]

EYOPAH

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget