Habari | Afya | Makala | Magazeti | Michezo | Burudani | Teknolojia | Mapenzi

Mkubwa Fella amuonya Temba


Aliyekuwa Meneja wa Yamoto Band na Meneja wa Mkubwa na wanae, Said Fella 'Mkubwa Fella' amefunguka na kumuonya mmoja wa wasanii wake Mhe. Temba kuhusu aina ya nyimbo na tungo ambazo huwa anaziimba kwenye muziki wake. 
Fella amesema hayo wakati akimpongeza Chege Chinguda kwa video yake mpya 'Kaitaba' ambayo imefikisha watazamaji milioni 1 kupitia mtandao wa YouTube, Said Fella amesema kuwa sasa Temba amemaliza chuo hivyo yupo tayari kwa ajili ya kuleta kazi nyingine ila amemuonya juu ya kuimba matusi na kusema akijaribu kufanya hivyo kipindi hiki basi atafungiwa. 
"Mwanetu kamaliza chuo Mhe. Temba nae inabidi aje na ikibidi tuwambie wadau wafikishe ngoma town, wadau mbabe wa mdomo Temba washawasha anajiandaa akifika tunaomba support yenu muhimu sana naamini atabadilika na upepo ulipo kwa vijana na nimemwambia unajua muziki wa sasa awataki iyo iyo nini ipo apo down utafungiwa" alisema Fella 
Serikali kupitia Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limekuwa likifungia nyimbo pamoja na wasanii ambao wamekuwa wakikiuka utaratibu kwa kutoa nyimbo ambazo wao wanaona ni kinyume na maadili na utamaduni wetu. Hivi karibuni zaidi ya nyimbo 10 zilifungiwa kutopigwa kwenye vituo vya Radio na TV. 

Labels:
Reactions:

Post a Comment

[facebook][blogger]

EYOPAH

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget