Habari | Afya | Makala | Magazeti | Michezo | Burudani | Teknolojia | Mapenzi

Mbowe na Viongozi Wengine wa Chadema Washtakiwa kwa Makosa Nane Ikiwamo Uasi, Maandamano na Kuamasisha Chuki


MWENYEKITI wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na viongozi wengine watano wa chama hicho wamefikishwa katika Mahakama ya Kisutu na kusomewa mashtaka manane ikiwemo kufanya maandamano yaliyosababisha kifo cha Mwanafunzi wa Chuo cha NIT, Akwilina Akwiline, Feb 16 mwaka huu.

Watuhumiwa hao wamesomewa mashtaka hayo na Wakili wa Serikali, Faraja Nchimbi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri ambapo Nchimbi amedai kuwa kosa la kwanza ni kufanya mkusanyiko ama maandamano yasiyo na uhalali.

Washtakiwa wote kwa pamoja wanadaiwa Februari 16, 2018 wakiwa barabara ya Mkwajuni walikusanyika kwa lengo la kutekeleza mkusanyiko ili watu waliokuwepo eneo hilo waogope kuona maandamano ya kuvunja amani.

Kosa la pili ni kufanya mkusanyiko usio halali; washtakiwa wote wanadaiwa kutenda kosa hilo Februari 16, 2018 Barabara ya Kawawa maeneo ya Kinondoni Mkwajuni ambapo kwa pamoja wakiwa na watu wengine 12 ambao hawajafikishwa mahakamani wanadaiwa wakiwa katika maandamano na mkusanyiko wa vurugu waligoma kutii amri ya kusambaratika na kuvunja mkusanyiko huo uliosababisha kifo cha Akwilana Akwilini na majeraha kwa maofisa wa Polisi.

Kosa la tatu ni kuhamasisha chuki kwa wanajamii isivyo halali, ambalo linamkabili Mbowe, ambapo wanadaiwa Februari 16, 2018 akiwa Viwanja vya Buibui Kinondoni DSM akihutubia wakazi wa maeneo hayo na DSM alitoa matamshi ambayo yangesababisha chuki kwa Jamii.

Kosa la nne linalomkabili Mbowe ni uchochezi na kusababisha chuki katika jamii, ambapo inadaiwa alitenda Februari 16,2018. Inadaiwa akiwa Uwanja wa Buibui Kinondoni DSM akihutubia wakazi wa Dar alitoa matamshi  ambayo yangepelekea chuki katika Jamii huku kosa jingine likiwa ni la uchochezi wa uasi, ambapo inadaiwa Mbowe amelitenda Februari 16, 2018 katika viwanja vya Buibui Kinondoni DSM.

Inadaiwa akiwa na nia ya kupandikiza chuki na dharau dhidi ya uongozi uliopo madarakani alitoa maneno ambayo ni wazi yangesababisha uasi. Pia kosa jingine linalomkabili Mbowe ni uchochezi wa uasi, ambapo inadaiwa amelitenda Februari 16,2018 katika viwanja vya Buibui, Kinondoni DSM.

Inadaiwa akihutubia mkutano wa hadhara alitoa matamshi ambayo yangepandikiza chuki na dharau kwa wananchi wa Tanzania dhidi ya uongozi uliopo madarakani. Kosa la saba linamkabili Mbowe ambalo ni ushawishi wa utendekaji wa kosa la jinai, ambalo amelitenda Februari 16, 2018 maeneo ya Buibui Kinondoni DSM.

Inadaiwa Mbowe akiwa amejumuika na watu wengine aliwashawishi wakazi wa maeneo hayo na DSM kutenda kosa. Katika kosa la 8, Wakili Nchimbi amedai linamkabili Msigwa ambalo ni kushawishi raia kutenda kosa la jinai.

Msigwa anadaiwa ametenda kosa hilo Februari 16, 2018 katika viwanja vya Buibui Kinondoni DSM, ambapo aliwashawishi wakazi wa maeneo hayo na DSM kutembea mbele ya umma wakiwa na silaha.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, washtakiwa wote walikana ambapo Wakili Nchimbi amedai upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na anaomba tarehe kwa ajili ya kuwasomea maelezo ya awali. Hata hivyo, Wakili Nchimbi aliwasilisha maombi kwa mahakama hiyo ili washtakiwa wanyimwe dhamana kwa sababu ya usalama wa umma wa Watanzania. 
Reactions:

Post a Comment

[facebook][blogger]

EYOPAH

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget