Habari | Afya | Makala | Magazeti | Michezo | Burudani | Teknolojia | Mapenzi

Waasi Sudani Kusini wakataa kuwaachilia marubani Wakenya bila ya malipo


Afisa wa kundi la waasi Sudan kusini amepuuzilia mbali taarifa kuwa wameitisha $200,000 ili wawaachilie huru marubani wawili wa Kenya wanaozuiwa katika eneo la Akobo, kaskazini mwa jimbo la Upper Nile.
Waasi hao waliwazuia marubani hao wawili baada ya ndege yao kuanguka, na kusababisha kifo cha mtu mmoja na ng'ombe kadhaa.
Hatahivyo waasi hao wanasema wanachotaka ni kulipwa fidia kwa hasara iliyotokana na vifo hivyo.
Kwa mujibu wa ripoti kutoka televisheni inayomilikiwa na serikali, Utawala wa rais Salva Kiir Serikali ya Sudan kusini imewataka wawachilie marubani hao pasi masharti yoyote.
"Serikali imetaka vikosi vya waasi katika jimbo la Akobo viwaachilie huru Wakenya wawili wanaowazuia bila masharti yoyote," alisema mtangazaji wa TV.
Taarifa ilisema kuwa waziri wa uchukuzi John Luke Jok ametuma kikosi kuchunguza ni nini kilichosababisha ajali hiyo ya ndege.
Gazeti la Sudan Tribune linaripoti kuwa Kanali Lam Paul Gabriel katika mahojiano na gazeti hilo Jumatano, alikana taarifa za vyombo vya habari kuwa gavana aliyeteuliwa wa waasi Koang Rambang aliitisha kikombozi ili kuwaachilia marubani hao wa Kenya.
Kanali Lam alithibitisha kuwa wanawazuia marubani hao tangu ndege hiyo ilipoanguka Januari 9 lakini alikana kuwa wametekwa na vikosi vya waasi wa SPLA-IO, linaripoti Sudan Tribune.
Mtu mmoja aliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa wakatindege hiyo ilipoanguka.
Waasi hao wanaomtii aliyekuwa makamu wa kwanza rais Riek Machar wamesema hawatowaachilia raia hao wawili wa Kenya hadi familia iliopoteza jamaa yake katika ajali hiyo ilipwe fidia.
Reactions:

Post a Comment

[facebook][blogger]

EYOPAH

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget