Habari | Afya | Makala | Magazeti | Michezo | Burudani | Teknolojia | Mapenzi

Tetesi za soka Ulaya Leo Jumatatu 22.01.2018


Mshambuliaji kutoka Chile Alexis Sanchez amepigwa picha akiwa amevaa jezi ya Manchester United kwa mara ya kwanza huku akikaribia kuhamia Old Trafford kutoka Arsenal. (Metro)
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amesema uhamisho wa Sanchez kutoka Arsenal kwenda United ulichochewa na 'tamaa' ya fedha. (Telegraph)
Arsene Wenger amekiri kuwa wasiwasi kuhusu mustakabali wa Sanchez Arsenal uliteteresha morali ya timu nzima. (Guardian)
Kiungo wa Arsenal Mesut Ozil, 29, anakaribia kupewa mkataba mpya iwapo timu hiyo itafanikiwa kumsajili Pierre-Emerick Aubameyang, 28, kutoka Borussia Dortmund, pamoja na Henrikh Mkhitaryan, 29, kutoka Manchester United. (Sun)
Mkurugenzi mkuu wa Arsenal Ivan Gazidis ameonekana mjini Dortmund huku akijaribu kukamilisha uhamisho wa Pierre-Emerick Aubameyang. (Express)
Olivier Giroud atajiunga na Borussia Dortmund kwa mkopo hadi mwisho wa msimu iwapo Pierre-Emerick Aubameyang atakamilisha uhamisho wake kwenda Emirates. (Kicker)
Cristian Pavon ameonesha dalili za kuondoka Boca Juniors na kwenda Arsenal. (Goal)
Mkurugenzi wa michezo wa Roma, Monchi amesema kuna uwezekano Chelsea wakawasajili Edin Dzeko, 31 na beki Emerson Palmieri, 23. (Metro)
Roma tayari wana mipango ya kuziba pengo la Dzeko na Emeron iwapo watahamia Chelsea. (Goal)
Chelsea huenda wakamsajili Peter Crouch, 36, licha ya meneja wake Paul Lambert kusisitiza kuwa mshambuliaji huyo hauzwi. (Independent)
Meneja wa Chelsea Antonio Conte amekiri kuwa Mitchy Batshuayi huenda akaondoka Darajani mwezi Januari. (Goal)


Mshambuliaji wa Burnley Asley Barnes, 28, ananyatiwa na meneja wa Chelsea Antonio Conte, huku meneja huyo akiendelea kutafuta mshambuliaji. (Sky Sports)
Manchester United watakuwa na wasiwasi baada ya kipa wa Athletic Bilbao Kepa Arrizabalaga kukataa nafasi ya kujiunga na Real Madrid, na hivyo huenda Real wakarejea kutaka kumsajili David de Gea, 27. (Mirror)
Cristiano Ronaldo huenda akawa tayari kupunguziwa mshahara ili kuondoka Real Madrid na angependa kurejea Manchester United. (Don Balon)
Baada ya kuacha kumfuatilia Thomas Lemar, Liverpool sasa wanataka kumsajili mchezaji wa Kimataifa wa Marekani Christian Pulisic. (Daily Star)
Rais wa chama cha soka cha Misri amesema angependa kuona Mohamed Salah akijiunga na Real Madrid. (The Sun)
Liverpool itamruhusu Daniel Sturridge kuondoka Anfield mwezi Januari. (Sky Sports)
Arturo Vidal, 30, amesema "hakuna uwezekano" wa yeye kuondoka Bayern Munich mwezi Januari, huku Chelsea ikihusishwa na kiungo huyo kutoka Chile. (Goal)
Mauricio Pochettino amesema Tottenham haina mpango wa kumfuatilia winga wa Bordeaux Malcolm. (Goal)

Mkuu wa akademi ya Manchester City Brian Marwood amekwenda kumtazama kiungo wa Lille Boubakary Soumare, 18, ambaye ametajwa kuwa ni "Paul Pogba mpya". (Mail)


Manchester City wanafikiria uwezekano wa kupeleka wachezaji wao chipukizi kwenda kwa mkopo katika klabu ya Bristol City ambao watakutana nao katika nusu fainali ya Kombe la Ligi. (Mirror)
Manchester City waliacha kumfuatilia Alexis Sanchez ili kumfuatilia Fred. (Daily Star)
Kiungo Kevin De Bruyne anatarajiwa kupewa mkataba mpya Manchester City kutokana na kuonesha kiwango kikubwa. (BBC Sport)
Nyota wa Real Madrid Gareth Bale ameshawishiwa kwa dau la euro milioni 100 ili kujiunga na Bayern Munich. (Don Balon)
Meneja wa Newcastle Rafael Benitez ameiambia klabu yake kuwa hatojadili kuhusu kuongeza mkataba wake mpaka baada ya dirisha la usajili kufungwa mwezi Januari. (Telegraph)


Labels:
Reactions:

Post a Comment

[facebook][blogger]

EYOPAH

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget