Habari | Afya | Makala | Magazeti | Michezo | Burudani | Teknolojia | Mapenzi

Tetesi za soka Ulaya leo Jumatano 24.01.18


Arsenal imeongeza kitita cha fedha kulipa kumsajili mchezaji wa Borussia Dortmund ambaye ni raia wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, mwenye umri wa miaka 28, kutoka pauni milioni 48.3 hadi pauni milioni 50.9. (Bild)
Mtaalamu wa soka ya Ujerumani Raphael Honigstein ana amini azma ya Arsenal kumsajili Aubameyang itategemea iwapo klabu hiyo ya Ujerumani itaweza kumpokea mshambuliaji wa Gunners mwenye umri wa miaka 31 Olivier Giroud kwa mkopo kwa wakati uliosalia msimu huu. (BBC Radio 5 live)
Arsenal pia inaazimia kumsajili mlinzi wa kiungo cha kati wa West Brom Jonny Evans. Raia huyo wa Ireland Kaskazini anakataa kusaini mkataba mpya na The Hawthorns. (Mirror)
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho anamtaka mchezaji wa kiungo cha kati wa timu ya Nice raia wa Ivory Coast Jean Michael Seri, 26. (Sun)
Aliyekuwa mkufunzi wa Manchester United Louis van Gaal nimojawapo ya wagombea wanaopigiwa upate kuwa mkuu wa timu ya taifa ya Australia (Telegraph)
Mshambuliaji wa Atletico Madrid na Argentina Nicolas Gaitan, mwenye umri wa miaka 29, atalipwa pauni 120,000 kwa wiki ili ajiunge na Swansea. (sun)


Manchester City wanafikiria kumfukuzia mchezaji wa kiungo cha beki katikati wa timu ya Atletico Bilbao Aymeric Laporte, mwenye umri wa miaka 23, na mchezaji wa kiungo cha kati wa Shakhtar Donetsk, raia wa Brazil Fred, 24. (Guardian)
Raheem Sterling atakuwa mchezaji wa hivi karibuni wa Manchester City kupewa mkataba wa muda mrefu. Mkataba wa mchezaji huyo wa kiungo cha mbele raia wa England ni wa thamani ya £275,000 kwa wiki. (Mirror)
Real Madrid wanamfukuzia kwa mara nyingine kipa wa Manchester United David de Gea, mwenye umri wa miaka 27. Timu hiyo ya Uhispania pia inaarifiwa kumfukuzia kipa wa Chelsea raia wa Ubelgiji Thibaut Courtois. (Marca)
Liverpool imeanza mazungumzo ya kumsajili Luan, wa timu ya Gremio. Raia huyo wa Brazil anasatihili kulipiwa pauni milioni 16 kwa mujibu wa kandarasi yake ili aruhusiwe kuhama. (Yahoo Sport)


West Brom wana hamu ya kumsajili aliyekuwa mchezaji wa kiungo cha mbele wa Chelsea Andre Schurrle, mwenye umri wa miaka 27, kwa mkopo.
Borussia Dortmund wapo tayari kulipa sehemu ya mshahara wa raia huyo wa Ujerumani wa £140,000 kwa wiki. (Mail)
West Brom wana hamu ya kumsajili mshambuliaji wa Bournemouth raia wa DR Congo Benik Afobe, mwenye umri wa miaka 24. (Sky Sports)
Mshambuliaji wa zamani wa Brazil Ronaldo, anatafakari kuhusu kununua timu ya kiwango cha pili Uingereza au Uhispania. (Folha de S. Paulo, via Mail)
Huenda mchezaji wa zamani wa Leeds United Ross McCormack akarudi Elland Road. Mshambuliaji huyo wa Uskochi ni mojawapo ya wachezaji wawili wa Aston Villa walioivutia timu hiyo. Mwingine ni mlinzi Tommy Elphick, mwenye umri wa miaka 30. (Yorkshire Post)


Labels:
Reactions:

Post a Comment

[facebook][blogger]

EYOPAH

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget