Habari | Afya | Makala | Magazeti | Michezo | Burudani | Teknolojia | Mapenzi

Tetesi za soka: Hazard, Aubameyang, Pastore, Ozil, Evans


Manchester City wako tayari kutoboa mfuko wao kwa kitita cha Euro milioni 150 kummendea mchezaji wa Chelsea Eden Hazard, mwenye umri wa miaka 27, baada ya Pep Guardiola kumbaini winga wa Ubelgiji kama mchezaji muhimu atakaemtia kibindoni wakati wa majira ya joto kulingana na gazeti la Sunday Mirror
Arsenal lazima itimize kiwango cha Borussia Dortmund cha Euro milioni 60 inachokitaka kama bei ya kumnunua Pierre-Emerick Aubameyang, mwenye umri wa miaka 28, ama itafute kwingine, linasema gazeti la Sunday Mirror
Wakati huo huo mwenyekiti Paris St-Germain Nasser Al-Khelaifi anasesema uvumi kuwa Neymar, mwenye umri wa miaka 25, anahamia Real Madrid unamfanya acheke na akasisitiza kwa asiliia "2,000%" kwamba mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Brazil atakuwa ndani ya jezi ya Ligue 1 msimu ujao, kulingana na gazeti la Mail la Jumapili
Manchester City na Manchester United wanatarajia kung'ang'ana kujaribu kumchukua mchezaji wa kati mBrazil Fred mwenye umri wa miaka 24, kutoka Shakhtar Donetsk limesema kazeti la Daily Star Jumapili.
Liverpool na Tottenham wanatarajia kumkosa kiungo wa kati wa timu ya Ufaransa -Paris St-Germain Javier Pastore, mwenye umri wa miaka 28 ambaye amethibitisha kuwa kurejea Italia ndio chaguo lake, limesema gazeti la Metro.
Na hali si mbaya sasa kwa Mesut Ozil mwenye umri wa miaka 29, ambae masaibu yake yamekwisha , kufuatia kuondoka kwa Alexis Sanchez kutoka Arsenal hadi Manchester United, linabainisha gazeti la Manchester Evening News
Nalo gazeti la Mail la Jumapili limetangaza kuwa ni wazi sasa meneja wa zamani wa Barcelona Luis Enrique ndie mgombea aliye mstari wa mbele katika kinyang'anyiro cha kumrithi Antonio Conte, ambae hali yake ya baadae katika kilabu hicho imo mashakani katika kipindi cha msimu wa majira ya joto.


Chelsea nao wako tayari kuboresha zaidi mipango yao kujaribu kukamilisha utaratibu wa kusaini mkataba na mshambuliaji wa zamani wa Manchester City Edin Dzeko kutoka Roma, kulingana na Sunday Express.
Wakati huo huo gazeti la Daily Star la Jumapili limethibitisha kuwa Arsenal wamepania kushinda mchuano wa kutia saini mkataba na mlinzi wa West Brom Jonny Evans, mwenye miaka 30, huku Manchester City wakiwa na uhakika wa kusaini mkataba na Aymeric Laporte kutoka Athletic Bilbao.
Burnley boss Sean Dyche anataka mlinzi wa Arsenal Rob Holding, mwenye umri wa miaka 22, kwa deni kwa kipindi cha msimu kilichosalia, lakini mkataba huo unaweza kutegemea iwapo Gunners wako tayari kusaini mkataba na Jonny Evans kulingana na gazeti la Sun la Jumapili.
Roma kwa upande mwingine imepinga nia ya Liverpool ya kumtaka mlinda lango wa Brazil Alisson Becker mwenye miaka 25, limesema gazeti la Metro.
Newcastle wako tayari kuipiku Liverpool kwa kutia saini na mBrazil Luan, 24, kutoka Gremio kwa Euro milioni 17, kulingana na gazeti la Sun


Wakala wa Jorginho wamekutana na wawakilishi wa Manchester United kabla ya kuondoka kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 kutoka Napoli, kulinga na jarida la habari la Manchester
Sunday Express, linasema Manchester United wanatarajiwa kukataa kusaini mkataba na mchezaji kutoka Juventus na Roma Matteo Darmian, mwenye miaka 28, kwa deni .
Tottenham itaendelea kufanya mazungumzo na Paris St-Germain juu ya uwezekano wa kusaini mkataba wa Euro milioni 22 kwa ajili ya usajiri wa kijana Lucas Moura mwenye umri wa miaka 25 kulingana na Sunday Telegraph
Leicester striker Leonardo Ulloa, mwenye miaka 31, anaripotiwa kukamilisha deni lake na kurejea tena kwenye kilabu chake cha zamani cha Brighton, linasema gazeti la Leicester Mercury.
Feyenoord ameweka muda wa mwisho kwa Newcastle wa kukamilisha malipo yake ya Euro milioni 20 zinazotakiwa kumnunua mshambuliaji wa Denmark Nicolai Jorgensen mwenye umri wa miaka 27, kulingana na jarida la Newcastle Chronicle
Newcastle na Crystal Palace wanapania kumnunua mchezaji wa kikosi cha Red Star Richmond Boakye, mwenye miaka 24.
Labels:
Reactions:

Post a Comment

[facebook][blogger]

EYOPAH

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget