Habari | Afya | Makala | Magazeti | Michezo | Burudani | Teknolojia | Mapenzi

Scorpion ahukumiwa kifungo cha miaka saba na Fidia ya Milioni 30


Mahakama ya Wilaya ya Ilala leo Jumatatu Januari 22, 2018 imemhukumu Salum Njwete maarufu kama ‘Scorpion’ kifungo cha miaka saba jela na kulipa fidia ya Sh30 milioni itakayotakiwa kulipwa kwa haraka.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Flora Haule amesema ameridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka, hivyo amemtia hatiani mshtakiwa chini ya kanuni ya adhabu kifungu cha 225 kama kilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2007.

Haule amesema kutokana na ushahidi uliotolewa, mahakama imejiridhisha kumtia hatiani Njwete  kwa kosa la kujeruhi pamoja na wizi.

Baada ya hakimu kumaliza kupitia hoja za pande zote mbili, wakili wa Serikali  Frank Tawali aliomba mahakama itoe adhabu stahiki kwa kuwa Njwete  alimtoboa macho, Saidi Mrisho ambaye alikuwa akitegemewa na familia yake na Taifa.

Wakili wa mshtakiwa,  Hussein Hitu aliiomba mahakama kumpunguzia mteja wake adhabu kwa kuwa ameshakaa rumande kwa muda mrefu, lakini pia ana familia inayomtegemea.

Njwete (35) alikuwa akituhumiwa kufanya unyang’anyi wa kutumia silaha na kujeruhi ikiwemo kumtoboa macho Mrisho.
Reactions:

Post a Comment

[facebook][blogger]

EYOPAH

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget