Habari | Afya | Makala | Magazeti | Michezo | Burudani | Teknolojia | Mapenzi

Rais Magufuli Kuzindua Pasipoti ya Kielektroniki


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. John Pombe Magufuli leo  atazindua Pasipoti Mpya ya Tanzania ya kielektroniki jijini Dar es Salaam.

Uzinduzi huo utafanyika Jumatano, Januari 31, 2018 kuanzia saa moja na nusu asubuhi, Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji, Kurasini Dar es salaam.

Hayo yalisemwa na Mrakibu wa Uhamiaji ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Ali Mtanda katika mahojiano maalum na Idara ya Habari (MAELEZO).

Mtanda alisema kuwa Pasipoti Mpya ya Tanzania ya kielektroniki ni sehemu ya Mfumo wa Uhamiaji Mtandao ambao utakuwa na visa, vibali mbali mbali na manejimenti mipakani.

Kwa kuwa teknolojia inazidi kukua, Tanzania haiwezi kubaki nyuma ndiyo maana imeamua kuingia katika masuala ya digiti.

Uzinduzi huu utahudhuriwa pia na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein.

Marais wastaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, waheshimiwa, Ali Hassan Mwinyi, Benjamin William Mkapa na Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wengine wa Serikali wanatarajiwa kuhudhuria uzinduzi huo kwa mujibu wa Mtanda.

Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati katika kutoa huduma zake kwa wananchi kwa njia ya mtandao. Ikumbukwe kuwa usajili wa makampuni chini ya Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) wamezindua usajili wa makampuni kwa njia ya mtandao, miamala ya pesa inafanyika kwa kiwango kikubwa kwa njia ya mtandao na kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi ikiwepo kulipa kodi mbali mbali.
Reactions:

Post a Comment

[facebook][blogger]

EYOPAH

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget