Habari | Afya | Makala | Magazeti | Michezo | Burudani | Teknolojia | Mapenzi

Je Man City itanyanyua mataji manne katika msimu mmoja?


Baada ya ushindi wa Manchester City dhidi ya Bristol City katika taji la Carabo, je matumaini ni yapi kwa timu hiyo kupata ushindi wa mataji manne mtawalia katika msimu mmoja?
Mkufunzi wa Mancity Pep Guardiola sasa amesalia na mechi moja kufikia ushindi wa taji lake la kwanza la fedha akiwa katika timu hiyo, baada ya kuvumilia ukame wa msimu wa pili tangu awe mkuu wa timu hiyo mnamo 2016-17.
Mhispania huyo mwenye umri wa miaka 47, aliyeshinda mataji 14 katika miaka minne kama mkufunzi wa timu ya Barcelona, na mataji saba zaidi katika miaka mitatu akiongoza Bayern Munich, anatarajia kuiongoza ManCity kwa ushindi wa mataji manne mtawalia katika msimu mmoja.
Licha ya kupuuzia uwezo wa timu yake kupata ushindi huo, miamba ya Mancity imeendelea kujizatiti katika nyanja zote - ikiwa tayari inaongoza kwa pointi 12 za wazi mbele katika ligi ya England, wamefanikiwa pia kufuzu kuwa katika orodha ya timu 16 katika ligi ya mabingwa na wapo katika awamu ya nne ya kombe la FA.
Iwapo watafanikiwa kufuzu na kuingia katika robo fainali za ligi ya mabingwa, hata katika kiwango hichi cha awali , huedna wana nafasi bora ya kufagia ligi na mataji.


Hatua muhimu kwa Pep - Takwimu

Pep Guardiola alisherehekea ushindi wake wa 363 katika uongozi wa juu katika mchezo wake wa 500, huku ushindi wa mara 63 ukitokana na mechi 92 na Manchester City.
Guardiola ameshinda mechi 11 ya jumla ya mechi 18 za nusu fainali, na kufanikiwa kufuzu kwa fainali yake ya kwanza kama meneja England.
Manchester City wamefuzu kwa fainali yao ya sita katika League Cup na kushinda manne kaiya matano ya awali - 1970, 1976, 2014 na 2016.
Ni kwa mara ya nne sasa Man City imefuzu kuingia katika fainali ya kuliwania taji nyumbani katika misimu sita iliyopita na kufanikiwa kushinda taji la League Cup mnamo 2014 na 2016, pamoja na kuishia kuwa mshindi wa pili katika kombe la FA mnamo 2013.

Nini kinafuata?

Bristol City inaendelea kujitahidi kukwea katika Premier League wanapoikaribisha QPR Jumamosi, 27 January (18:00 ). Huku Manchester City, wapo ugenini kwa mabingwa Cardiff City katika awamu ya nne ya komba la FA Jumapili 28 January (19:00 ).

Labels:
Reactions:

Post a Comment

[facebook][blogger]

EYOPAH

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget