Habari | Afya | Makala | Magazeti | Michezo | Burudani | Teknolojia | Mapenzi

Federer amchakaza Marin Cilic katika fainali za Australian Open na kuifikia rekodi ya Serena Williams


Mcheza tenisi nguli duniani Roger Federer ameifikia rekodi ya wacheza tenisi watatu ya kutwaa mataji 20 ya (Grand Slam) baada ya kushinda taji la mashindano ya wazi ya Australia mchana huu.
Federer amefikia mafanikio hayo baada ya kumshinda Marin Čilić wa Croatia kwa seti 6-2 6-7 (5-7) 6-3 3-6 6-1 katika fainali iliyomalizika mchana huu jijini Melbourne Australia.
Nyota huyo raia wa Uswis mwenye miaka 36, amewafikia nyota wa tenisi Serena Williams wa Marekani, Margaret Court wa Australia na Steffi Graf wa Ujerumani ambao wameshinda mataji 20 ya Grand Slam kila mmoja.

Federer pia amewafikia Novak Djokovic na Roy Emerson ambao kila mmoja ametwaa mara sita ubingwa wa michuano ya wazi ya Australia kwa upande wa wanaume.
Baada ya kushinda mchezo huo wa fainali Federer amesema amefurahi sana na taji hilo limemwongezea nguvu ya kuendelea kusaka mafanikio zaidi licha ya umri wake kuanza kumtupa mkono.
Labels:
Reactions:

Post a Comment

[facebook][blogger]

EYOPAH

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget