Habari | Afya | Makala | Magazeti | Michezo | Burudani | Teknolojia | Mapenzi

Mwaka 2018 nataka na mimi niitwe Mama – Gigy Money


Msanii wa muziki ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Nampa Papa’, Gift Stanford maarufu kama Gigy Money, amedai kuwa yupo mbioni kupata mtoto, baada ya mastaa mbalimbali kufanikiwa kupata watoto hivi karibuni.

Msanii huyo anayefanya vyema na kibao chake hicho, amesema amefikia wakati wa kuitwa mama na Mungu akipenda mwakani anatamani hilo litimie.
“Kuitwa mama ni baraka na hakuna mwanamke ambaye hatamani hilo, kikubwa ni mipango tu kwa kuwa huwezi kukurupuka, halafu kingine mtoto ni mipango ya Mungu, unaweza kupanga hivi ikawa vile, sasa naona na mimi ni wakati wangu wa kutimiza hilo,” Gigy aliliambia Gazeti la Mtanzania.
Alisema pamoja na malezi kuwa na changamoto zake lakini ni jambo ambalo lazima alipitie na amejipanga vyema kutimiza azma yake hiyo aliyojiwekea na mpenzi wake.
Gigy alisema anatarajia kupata mtoto na mpenzi wake wa siku nyingi ambaye wote kwa pamoja wameridhia jambo hilo.

Labels:
Reactions:

Post a Comment

[facebook][blogger]

EYOPAH

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget