Habari | Afya | Makala | Magazeti | Michezo | Burudani | Teknolojia | Mapenzi

Erasto Nyoni Atangazwa Mchezaji Bora Mwezi Oktoba


MCHEZAJI kiraka wa Simba, Erasto Nyoni ametangazwa kuwa mchezaji bora wa timu hiyo wa wa mwezi Oktoba.

Hiyo ni baada ya kuonyesha kiwango kikubwa kwenye mechi nne za Ligi Kuu Bara ambacho amezicheza huku akisaidia timu yake kupata matokeo mazuri.

Kiraka huyo, alijiunga na Simba kwenye msimu huu wa ligi kuu akitokea Azam FC mara baada ya mkataba wake kumalizika.
Nyoni akicheza nafasi ya beki wa pembeni namba mbili hadi sasa tayari ameitengenezea mabao matano katika mechi za ligi ambazo amezicheza.

Erasto ambaye anamudu kucheza nafasi nyingi uwanjani amekuwa chachu ya matokeo mazuri kwa timu ya Simba tangu asajiliwe akitokea Azam FC.

Mechi ambazo zimempa uchezaji bora katika mwezi huu hadi kupelekea kutwaa tuzo hiyo ya uchezaji bora ni dhidi ya Njombe Mji, Stand United, Mtibwa Sugar na Yanga kati ya hizo walishinda mbili na kutoa sare mbili.
mwisho.


Labels:
Reactions:

Post a Comment

[facebook][blogger]

EYOPAH

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget