Habari | Afya | Makala | Magazeti | Michezo | Burudani | Teknolojia | Mapenzi

Waziri Mwigulu atembelea ujenzi wa nyumba za Polisi Arusha

 

Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha
Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Mwigulu Nchemba leo mchana (Oktoba 17) amekagua eneo la ujenzi wa nyumba za Polisi jijini Arusha zinazoendelea kujengwa baada ya ajali ya moto iliyotokea mwishoni mwa mwezi Septemba ambayo ilisababisha familia za askari 13 kuunguliwa vitu mbalimbali na kukosa makazi.

Mwigulu alitumia fursa hiyo kwa kuishukuru kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa ambayo inaoongozwa na Mkuu wa mkoa Mh. Mrisho Gambo lakini pia aliwashukuru wadau ambao wote kwa pamoja walichukua hatua za haraka za kurejesha makazi ya askari ambao walikumbwa na janga la moto huku akisisitiza kwa kusema kwamba hali ilioonyeshwa na wadau hao ni mfano mzuri wa kuigwa na mikoa mingine waone nchi inajengwa na wananchi.

Alisema kwamba suala la makazi ya askari lipo katika kipaumbele cha serikali na Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameonyesha kwa vitendo katika maeneo tofauti ikiwemo hapa Arusha.

Alisema Serikali ikishamaliza hilo itaendelea na utaratibu mwingine wa kujenga majengo ya kisasa ili askari wapate makazi bora huku akimuagiza Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha awafikishie salamu askari wa Arusha kwamba, Mh. Rais yupo pamoja nao na Wizara ipo pamoja nao.

Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles Mkumbo mbali na kuendelea kuwashukuru wadau hao kwa kujitolea na kumuunga mkono Mh. Rais ambaye alionyesha njia siku hiyo hiyo usiku kabla hakujapambazuka kwa kutoa mchango wake kama Serikali, lakini pia alisema bado milango ipo wazi kwa watu wengine ambao hawakuwa na taarifa juu ya tukio hilo ili kulisaidia Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha liweze kufanikisha ujenzi wa makazi ya askari hao.

Kamanda Mkumbo aliongeza kwa kusema ujenzi wa makazi bora ya askari mkoani hapa utasaidia kuwaongezea morali zaidi wa kazi askari hao hali ambayo itazidi kuimarisha usalama na shughuli za maendeleo kusonga mbele.

Jumla ya nyumba 29 za askari katika moja ya kambi iliyoathirika na ajali ya moto zilianzwa kujengwa toka tarehe 2 mwezi huu jijini hapa na saba ambazo zipo katika ngazi ya msingi zinatarajiwa kujengwa katika kituo kidogo cha Polisi Morombo kata ya Murieti.


Reactions:

Post a Comment

[facebook][blogger]

EYOPAH

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget