Habari | Afya | Makala | Magazeti | Michezo | Burudani | Teknolojia | Mapenzi

Idadi ya watu waliouawa kwenye shambulizi Mogadishu yafika 300


Idadi ya watu waliouawa kwenye ,lipuko mkubwa wa bomu katika eneo lenye shughuli nyingi kwenye mji mkuu wa Somalia Mogadishu siku ya Jumamosi, imefikia watu 300 hadi sasa, kwa mujibu wa ripoti ya shirika la hahari la Reuters
Takriban watu wengine 300 walijeruhiwa kwa mujibu wa AFP, wakati lori lililokuwa limejazwa milipuko lilipolipuka karibu na lango la hoteli.
Reuters walimnukuu Ahmed Ali, muuguzi anayefanya kazi kwenye hospitali moja akisema kuwa miili 160 haikuweza kutambuliwa na hivyo ilizikwa na serikali jana.
Anasema kuwa miili mingine ilizikwa na jamaa zao.
Hilo ndilo shambulizi baya zaidi kutokea nchini Somalia tangu kundi la al-Shabab lianzishe harakati zake mwaka 2007.
Rais Mohamed Abdullahi "Farmajo" Mohamed alilaumu kundi la al-Shabab kwa shambulizi hilo katili.
"Tumethibitisha kuwa watu 300 waliuawa kwenye mipuko huo. Idasi ya waliokufa huenda bado ikaongezeka na kuna watu kadha ambao bado hawajulikani waliko," Abdikadir Abdirahman, mkurugenzi wa idara ya magari ya kusafirisha wagonjwa aliliambia shiria la Reuters.
Reactions:

Post a Comment

[facebook][blogger]

EYOPAH

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget