Habari | Afya | Makala | Magazeti | Michezo | Burudani | Teknolojia | Mapenzi

Yanga yaipeleka Takukuru kamati ya saa 72 ya TFF kuhusu point 3 za Simba SC na Kagera Sugar

 

Uongozi wa klabu ya Yanga umesema umepeleka taarifa kwenye taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Takukuru na Jeshi la Polisi ili kufuatilia mwenendo wa utendaji kazi wa kamati ya saa 72 ya TFF.

Mjumbe wa kamati ya utendaji ya Yanga, Salum Mkemi alisema wana wasiwasi na kamati hiyo inaweza kuipa Simba pointi tatu kutokana wajumbe wake wengi kuwa wanachama wa Simba.

“Sisi ni mabingwa na tuna haki ya kulinda maslahi yetu, Simba walipokea kichapo lakini wanataka ushindi wa mezani, suala hili tunalipinga. Tunaambiwa kamishna wa mchezo na mwamuzi wameitwa kutoa ushahidi.Tumeshawasiliana na mamlaka za kuzuia na kupanga na rushwa ili waichunguze kamati hii,”aliseleza Mkemi.

Mkemi aliwataja wajumbe wa kamati hiyo Msafiri Mgoyi, Baruani Muhuza na Boniface Wambura aliodai ni wanachama wa kugalagala wa Simba hivyo hivyo uwepo wao katika kamati hiyo utaathiri maamuzi yatakayotolewa.

“Tunawaambia mpira unatakla kuharibika, wasithubutu kuipa Simba pointi 3, pointi za Kagera zina maslahi kwetu kama Yanga,”alisema Mkemi na kuitupia lawama kuwa inaongoza kwa mchezo wa kughushi nyaraka.

Mkemi ambaye katika mkutano huo aliambatana na Katubu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa.

Kanuni ya 16 (C) ya Ligi Kuu inasema “Kamati husika itaketi kusikiliza na kuitolea uamuzi Rufaa hiyo baada ya kupata vielelezo husika na wajumbe wa Kamati hiyo kukamilika. Mkata rufaa atawasilisha vielelezo kuhusu rufaa yake, rufaa isiyokuwa na vielelezo na ambayo haijalipiwa ada itatupwa.

Hata hivyo, Ofisa Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara alisema viongozi wa Yanga wanataka kuharibu mpira kwa kuingilia utendaji wa kamati na Bodi ya Ligi.

“Nimemsikia Mkemi lakini ningemshauri na wenzake wajikite kujenga uwanja wao na kulipa mishahara ya wachezaji. Sisi hatutaki kuingilia bodi ya ligi na kamati ya saa 72. Simba tunataka maamuzi ya haki na endapo kamati itafanya maamuzi kwa shinikizo tutajua Yanga inahusika, tuviache vyombo husika vifanye maamuzi,’alieleza Manara

Ofisa Habari na Mawasiliano wa (TFF) Alfred Lucas alizitaka pande mbili kusubiri uamuzi utakaotolewa na kikao cha kamati kitakachoketi kesho.

Labels:
Reactions:

Post a Comment

[facebook][blogger]

EYOPAH

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget